Karibu TUCASA MWECAU FAMILY
Sisi ni familia ya wanafunzi Wakristo katika Chuo Kikuu cha kikatoliki Mwenge (MWECAU), tunaounganishwa kwa imani yetu katika Yesu Kristo na tunalenga kuangaza nuru Yake katikati ya maisha ya chuo. Tunaamini kuwa maisha ya chuo sio tu ya kitaaluma, bali pia ni safari ya kiroho, ya kujifunza, kukua, na kushuhudia.
Katika familia ya TUCASA MWECAU, tunakukaribisha uwe sehemu ya:
Ibada za pamoja zenye kuinua moyo na kuimarisha imani.
Ushirika wa kweli wa wanafunzi wanaompenda Mungu.
Huduma za kiroho na kijamii zenye kugusa maisha ya watu.
Tunaamini kuwa kila kijana ana nafasi ya kipekee katika kazi ya Mungu. Tumejitoa kukuandaa kuwa mtumishi mwaminifu, kiongozi wa kesho, na mshuhuda hai wa Injili katika kila eneo la maisha yako.
Tunakualika:
Jiunge nasi kwenye ibada zetu za kila siku (jumatatu-alhamisi jioni hapa chuoni kwetu) na Ijumaa na Jumamosi Kanisani kariwa SDA.
TUCASA MWECAU FAMILY – Anchored In Christ Alone!
“Tazama, jinsi ilivyo vyema na kupendeza, Ndugu wakae pamoja kwa umoja!” – Zaburi 133:1